Yanga imefukia mashimo dirisha dogo

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
16 Jan 2026
Yanga imefukia mashimo dirisha dogo

Katika dirisha hili la usajili Yanga imeziba mashimo kwa kuboresha maeneo yaliyokuwa na changamoto tangu kuanza kwa msimu huu.

Wananchi wamemsajili 'kiungo chuma' Mohamed Damaro Camara 'Ngosha' ambaye hakuhitaji muda kudhihirisha ubora wake 'akikichafua' kwenye michuano ya kombe la Mapinduzi licha ya kuwa alikosa mchezo wa fainali akitumikia adhabu ya kadi nyekundu.

Moussa Balla Conte aliyesajiliwa katika eneo hilo kuchukua nafasi ya Khalid Aucho aliyetimkia Singida BS, mwanzo ilionekana kama amefeli lakini kupitia michuano ya kombe la Mapinduzi nae ameonyesha umahiri wake ambao haukuwa umeonekana tangu alipojiunga na Yanga dirisha lililopita.

Eneo la kiungo cha ushambuliaji ameongeza 'Star Boy' Allan Okello kutoka klabu ya Vipers Fc ya Uganda.

Hili ni eneo ambalo aliondoka Stephane Aziz Ki, akaletwa Mohamed Doumbia ambaye hata hivyo ameanza taratibu na kupelekea uongozi kurudi sokoni kuimarisha eneo hilo.

Safu ya ushambuliaji Yanga imeongeza washambuliaji wawili Emmanuel Mwanengo ambaye ni mchezaji wa ndani na Laurindo Dilson Maria Aurelio 'Depu' aliyetua kutoka Poland.

Depu ni mchezaji mwenye cv kubwa zaidi miongoni mwa nyota waliosajlliwa na Yanga katika dirisha hili.

Licha ya kuitumikia kwa mafanikio klabu ya Petro Atletico na timu ya Taifa ya Angola, Depu amecheza timu za ligi kuu barani Ulaya katika nchi za Ureno na Poland.

Kitendo cha Yanga kumrejesha Afrika mshambuliaji huyo, kinaonyesha dhamira ya Wananchi kufanya vyema hasa kwenye ligi ya mabingwa.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
13h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’