Msimu huu 2025/26 Maxi Nzengeli ameendelea kuutendea haki juzi akibeba tuzo ya mchezaji bora wa michuano ya kombe la Mapinduzi.
Maxi alibeba tuzo hiyo baada ya kuwa na mashindano bora, Yanga ikiibuka mabingwa, ushindi wa mikwaju ya penati 5-4 dhidi ya Azam Fc baada ya dakika 120 za kutofungana.
Mkufunzi wa Yanga Pedro Goncalves kwa sasa anamtumia Maxi eneo la kiungo zaidi ambapo Mcongomani huyo tangu alipobadilishiwa majukumu anaonekana kuwa bora zaidi.
Maxi ni mchezaji wa timu, mafanikio binafsi anayopata ni matokeo ya kazi nzuri anayoifanya katika kuipambania Yanga.



ADVERTISE HERE