Huyu Conte sio wa kutoa kwa mkopo

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
14 Jan 2026
Huyu Conte sio wa kutoa kwa mkopo

Ni wazi wakati huu viongozi wa Yanga watakuwa wanakuna vichwa juu ya wachezaji wa kigeni ambao wanapaswa kuondoka ili kupisha sajili za nyota wapya wa kigeni waliozikamilisha katika dirisha hili.

Kiungo Moussa Balla Conte alikuwa miongoni mwa wachezaji ambao walikuwa wakitajwa kwenye mpango wa kutolewa kwa mkopo.

Conte na Mohamed Doumbia walitajwa kuelekea Singida BS. Inawezekana mpango huo ukakamilika kwa Doumbia lakini Conte mambo yanaweza kubadilika.

Michuano ya kombe la Mapinduzi iliyofika tamati jana kwa Yanga kuibuka mabingwa wakishinda kwa mikwaju ya penati 5-4 dhidi ya Azam Fc baada ya suluhu ya bila kufungana, huenda ikawa imemsaidia Conte kubakisha nafasi yake Yanga.

Conte aliibuka nyota wa mchezo huo 'akiupiga mwingi' kwa dakika zote 120 na kuwaacha wengi na maswali ilikuwaje ubora huu haukuonekana tangu mwanzo alipotua?

Kiungo huyo raia wa Guinea alianza kuonyesha cheche zake kwenye mchezo wa nusu fainali dhidi ya Singida BS ambapo katika mchezo huo, mkufunzi wa Yanga Pedro Goncalves alimtumia kama beki wa kati.

Kukosekana kwa Mohamed Damaro kwenye mchezo wa fainali dhidi ya Azam Fc, Conte akarejea eneo la kiungo huko Dickson Job na Ibrahim Bacca wakianza eneo la mabeki wa kati.

Conte amedhihirisha anastahili kuendelea kusalia katika kikosi cha Yanga na anachohitaji zaidi ni nafasi ya kucheza.

Ikumbukwe mpaka sasa Yanga imewasajili Allan Okello na Laurindo Aurelio 'Depu' kama nyota wa kigeni huku Damaro akisajiliwa kama Mtanzania (alipata uraia mwaka 2025).

Andy Boyeli tayari ameondoka huku Doumbia akitajwa kuelekea Singida BS kwa mkopo. Ili kumrejesha Yao Kouassi kikosini Yanga itahitaji nafasi nyingine moja ya kigeni.

Conte 'gari limewaka', Frank Assink ameupiga mwingi tangu aaminiwe na Goncalves huku Celestin Ecua akiendelea kuaminiwa licha ya ukosoaji anaokumbana nao kutoka kwa mashabiki.

Ni wazi mazingira hayo yanaweza kuweka matatani hatma ya Yao ambaye anaendelea kuimarika baada ya kuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu. 

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
3h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
3h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
13h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
14h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
21h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’