Yanga imeendelea kukusanya mataji jana ikiandikisha taji la saba katika kipindi cha misimu miwili.
Ni baada ya ushindi wa mikwaju ya penati 5-4 dhidi ya Azam Fc kwenye mchezo wa fainali ya kombe la Mapinduzi ambao ulipigwa kwa dakika 120 na kumalizika kwa suluhu ya bila kufungana.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mh. Dk. Hussein Mwinyi aliwakabidhi Wananchi taji hilo baada ya mchezo huo uliopigwa kwenye uwanja ambao aliuzindua rasmi, Gombani, Pemba.





ADVERTISE HERE