Baada ya tetesi kuvuma kwa wiki kadhaa, hatimaye mashabiki wa Yanga leo watapokea zawadi ya Mapinduzi Day kutoka kwa Rais wa klabu yao, Injinia Hersi Said.
Majira ya saa 5 usiku Yanga itatambulisha usajili wa nyota mwingine anayejiunga na mabingwa hao wa soka Tanzania Bara katika dirisha hili.
Taarifa kutoka ndani ya uongozi wa Yanga imethibitisha kuna nyota wawili wa kigeni usajili wao umekamilika na wanachosubiri ni utambulisho.
Mshambuliaji wa kimataifa wa Angola, Laurindo Aurelio 'DepΓΊ' na kiungo mshambuliaji Allan Okello kutoka klabu ya Vipers Fc, Uganda.
Lakini utambulisho mkubwa unaosubiriwa zaidi huenda ukawa ule wa Okello ambaye amewasili nchini leo Jumatatu akitokea Uganda.
Hersi alisafiri yeye mwenyewe Uganda kukamilisha usajili wa Okello ambaye inaelezwa amepewa mkataba wa miaka miwili na nusu.