Mudathir, Mzize kuiwahi Al Ahly

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
10 Jan 2026
Mudathir, Mzize kuiwahi Al Ahly

Wachezaji Clement Mzize na Mudathir Yahya wanakaribia kurejea kwenye kikosi cha Yanga baada ya afya zao kuimarika.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amethibitisha kuwa nyota hao wameanza mazoezi ya timu wakielekea kurejea rasmi kikosini.

Mudathir na Mzize waliuanza msimu kwa kusuasua wakiandamwa na majeraha ya mara kwa mara.

Mzize alilazimika kufanyiwa upasuaji wa goti kufuatia majeraha aliyopata wakati akiwa kwenye majukumu ya timu ya Taifa katika michuano ya CHAN 2024 na kisha kujitonesha tena wakati Yanga ikijiandaa na mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Silver Strikers.

Nyota hao huenda wakawa tayari kuikabili Al Ahly katika mchezo wa raundi ya tatu kundi B ligi ya mabingwa barani Afrika.

Al Ahly na Yanga zitaumana katika mchezo utakaopigwa Januari 23 huko Misri kabla ya timu hizo kurudiana visiwani Zanzibar.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
3h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
3h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
13h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
14h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
21h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’