Nyika awatuliza mashabiki Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
31 May 2018
Nyika awatuliza mashabiki Yanga
Mwenyekiti wa kamati ya usajili ya klabu ya Yanga Hussein Nyika jana aliwatoa hofu mashabiki wa timu hiyo kwa kuwaeleza kuwa hakuna mchezaji ambaye yuko kwenye mipango ya kocha ataondoka.

Nyika alitoa kauli hiyo baada ya kuibuka kwa tetesi kwamba beki kisiki wa timu hiyo Kelvin Yondani amezima simu zake na hajulikani alipo.

Jana uongozi wa Yanga ulifanya kikao na wachezaji waliomaliza mikataba yao baada ya mazoezi ya asubuhi kabla ya safari ya Kenya leo.

Vilabu vya Simba, Azam FC na Singida United vinahusishwa kutaka kuwasajili baadhi ya nyota wa Yanga ambao mikataba yao inaelekea ukingoni.

Yondani amekuwa akiwindwa zaidi na vilabu vya Simba na Azam FC na inadaiwa mpango wa kuzima simu ulipendekezwa na viongozi wa Yanga.

Juma Abdul na Obrey Chirwa ni wachezaji wengine wanaohusishwa na vilabu vya Azam FC na Simba.

Nyika alisema wameongeza umakini kwenye zoezi la usajili baada ya kubaini kuna timu zinafuatilia nyendo zao ili kuwavurugia.

Yanga imekuwa ikiendesha zoezi la usajili 'kimyakimya' tofauti na timu nyingine.

Juzi msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara alitamba kuwa wamedhamiria kulipa kisasi kwa kuchukua wachezaji tegemeo kutoka Yanga huku akiahidi kwa mbwembwe kuwa watalipua bomu kabla hawajakwenda Kenya kushiriki mashindano ya SportPesa Super Cup.

Hata hivyo timu hiyo tayari imeelekea Kenya na hakuna mchezaji waliotangaza kumsajili kutoka klabu ya Yanga.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
7h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
11h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
16h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’