Goncalves anaitaka fainali kombe la Mapinduzi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
8 Jan 2026
Goncalves anaitaka fainali kombe la Mapinduzi

Kocha Mkuu wa Yanga Pedro Goncalves amesema amekiandaa kikosi chake kikamilifu kuhakikisha wanaibuka na ushindi kwenye mchezo wa nusu fainali kombe la Mapinduzi dhidi ya Singida BS utakaopigwa kesho Ijumaa.

Akizungumza katika mkutano na wanahabari mapema leo, Goncalves alisema haitakuwa mechi rahisi kwani zitakutana miongoni mwa timu nne bora zaidi nchini.

Licha ya ugumu wa mchezo huo, Goncalves amesema anaimani vijana wake watapambana na watatimiza malengo ya kufuzu hatua ya fainali.

“Kesho tunacheza na miongoni mwa timu bora hapa Tanzania, naamini timu zote bora zimefuzu hatua ya Nusu fainali na sasa kilichobaki ni sisi kutazama zaidi upande wetu ili tuweze kushinda kwasababu lengo letu kuu ni kufuzu hatua ya Fainali”.

“Tupo hapa kwaajili ya kutoa nafasi kwa wachezaji wetu wote ili waweze kuonesha uwezo wao na pia kuwapa nafasi wachezaji wapya ili wazoee mfumo wetu na mazingira yetu. Tunatambua Singida watatupa mechi ngumu lakini nina imani kwenye mchezo wa kesho tutafanya vizuri”.

“Tuna kikosi kikubwa kinachoweza kupambana na ninaimi kitatupa matokeo, ni kweli baadhi ya wachezaji muhimu hawapo na wengine ni majeruhi, lakini hawa tulionao wana uwezo mkubwa ndiyo maana wapo hapa, Bila shaka wapo tayari kwa changamoto ya kesho, tupo hapa kwaajili ya Kushinda,” alisema Goncalves.

Akizungumza kwa niaba ya wachezaji wenzake, beki chipukizi anayekuja kwa kasi Abubakar Nizar Othman 'Ninju' amesema wachezaji wote wako tayari kwa mchezo huo na watapambana ili kuhakikisha wanaibuka na ushindi.

“Sisi wachezaji tumejiandaa vizuri na tupo tayari, tunafahamu umuhimu wa mchezo wa kesho tunacheza na Singida ambao ni timu bora tunayocheza nayo ligi moja kule bara, kikubwa ni sisi kufuata maelekezo ya mwalimu ili kupata ushindi”

“Sisi pia tuna tahadhari kubwa kwasababu mchezo wa kesho ni muhimu sana, tunaweka tahadhari ya kutofanya makosa tukaadhibiwa, tunajua na wao wanatuhofia kwasababu wanaifahamu Yanga, niwaombe Mashabiki wetu waje kwa wingi hapo kesho ili tufurahi pamoja,” alisema

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
9h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
13h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
20h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’