Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' imeondoshwa kwenye michuano ya Afcon 2025 hatua ya 16 bora baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 dhidi ya wenyeji Morocco.
Bao la Brahim Diaz dakika ya 64 liliipa ushindi Morocco katika mechi ngumu ambayo vijana wa kocha Miguel Gamondi walipambana kwa jasho na damu.
Mwanzo ilionekana kama ingekuwa rahisi kwa Morocco inayoshika nafasi ya kwanza kwa ubora barani Afrika, lakini walichokutana nacho kutoka kwa Stars kilikuwa kitu tofauti.
Licha ya kuzuia kwa muda mwingi, Stars ilitengeneza nafasi adimu ambazo Simon Msuva na hata Feisal Salum kama wangekuwa makini wangeweza kufunga.
Aidha Stars ingeweza kupata mkwaju wa penati dakika za lala salama lakini VAR haikufanya kazi yake vyema katika tukio ambalo Idi Nado alifanyiwa madhambi.
Ilikuwa mechi ngumu, licha ya kupoteza mchezo huo, nyota wa Stars wameiheshimisha Tanzania