Baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya KVZ, Yanga inahitaji alama moja katika mchezo uliobaki dhidi ya TRA United ili kujikatia tiketi ya nusu fainali kombe la Mapinduzi.
Mabao ya Pacome Zouzoua, Ecua Celestin na Emmanuel Mwanengo yalitosha kuihakikishia Yanga ushindi muhimu katika mchezo wa kwanza kundi C.
Yanga itahitimisha hatua ya makundi kwa mchezo dhidi ya TRA United siku ya Jumanne, Wananchi wakihitaji ushindi au sare kutinga nusu fainali.



ADVERTISE HERE