Nyika akana kumsajili Ngassa, lakini ukweli ni kwamba..

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
30 May 2018
Nyika akana kumsajili Ngassa, lakini ukweli ni kwamba..
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga Hussein Nyika amekiri kwamba ni kweli mapema leo Jumatano, May 30 2018 winga wa Ndanda FC Mrisho Ngassa, alifika Makao Makuu ya klabu Yanga, Jangwani jijini Dar es salaam.

Hata hivyo bosi huyo wa masuala ya usajili amesema Ngassa alifika kuwasalimia viongozi wa klabu hiyo aliyowahi kuitumikia kwa mafanikio makubwa.

"Ile ilikuwa ni safari binafsi, amesema Nyika."

"Hakuna ukweli wowote kwamba Ngassa alikuja kukamilisha masuala ya usajili," amesisitiza.

Ngassa amekuwa akihusishwa kurejea Yanga na ukweli ni kwamba winga huyo tereza amerejea rasmi Jangwani.

Kwa muda wote aliokuwa Yanga Ngassa alikuwa ni kipenzi cha mashabiki wa timu hiyo.

"Najisikia furaha sana kwa sababu kila ninapokwenda huwa nakumbuka kwamba kuna mchango ambao ninao kwao na wao wanajua," amesema Ngassa baada ya kuthibitisha kuwa amerejea
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
9h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
12h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
15h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’