Sikupenda Aucho aondoke - Hersi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
27 Dec 2025
Sikupenda Aucho aondoke - Hersi

Mashabiki wa Yanga bado wanajiuliza nini kilitokea kwenye dirisha lililopita kupelekea aliyekuwa kiungo wao kipenzi Khalid Aucho maarufu daktari wa mpira kuondoka na kwenda kujiunga na Singida BS.

Aidha bado kuna kundi kubwa la mashabiki linatamani kuona kiungo huyo akirejea tena Yanga hasa kwenye dirisha dogo wakiamini pengo lake halijazibwa.

Rais wa Yanga Injinia Hersi Said amekiri haikuwa jambo rahisi ambalo hata yeye mwenyewe hakutamani litokee lakini wakati mwingine kuna mambo ya kimpira lazima yatokee.

"Aucho ni kiungo bora kuwahi kutokea Afrika Mashariki. Kama ingewezekana ningesema natamani Aucho kijana awepo kwenye timu yangu kwa miaka 20 ijayo"

"Ningetamani acheze Yanga muda mrefu, binafsi sikufurahishwa na sikutamani aondoke lakini ni jambo lilitokea tu," alisema Hersi

Aucho alisajiliwa na Singida BS kwa mkataba wa miaka miwili baada ya mazungumzo yake ya kuhuisha mkataba Yanga kutofikia mwafaka.

Yanga ilikuwa tayari kumpa Aucho mkataba wa mwaka mmoja wenye kipengele cha kuongeza mwaka wa pili mwishoni mwa msimu lkini nahodha huyo wa Uganda Cranes alitaka mkataba wa miaka miwili.

Licha ya kuondoka Yanga Aucho ameendelea kuwa na mahusiano mazuri na uongozi wa Yanga na pengine haitashangaza kuona akirejea tena kwa Wananchi kwa mara ya pili

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
10h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
15h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
19h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
20h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
20h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
21h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’