Habari njema kwa mashabiki wa Yanga ni kuwa wataendelea kumshuhudia beki Frank Assink akiwatumikia angalau hadi mwisho wa msimu baada ya Singida BS kukwama kumrejesha.
Assink anaitumikia Yanga kwa mkopo na tayari Singida BS waliomba mchezaji huyo arejeshwe kwenye kikosi chao.
Hata hivyo ni kama mpango huo umekufa baada ya matajiri hao kutoka Singida kusajili mabeki wawili Abdulmalick Zacharia kutoka Mashujaa Fc na Abdallah Kheri kutoka Pamba Jiji.
Assink sasa ataendelea kuwatumikia Wananchi hadi mkopo wake utakapomalizika na pengine Yanga huenda ikamsajiili moja kwa moja.
Beki huyo raia wa Ghana ameng'ara kwenye kikosi cha kocha Pedro Goncalves katika mechi mbili zilizopita na kujihakikishia nafasi yake ya kubaki Jangwani
ADVERTISE HERE