Licha ya Zimbabwe kupoteza mchezo wa kwanza wa Afcon 2025 kwa kufungwa mabao 2-1 dhidi ya Misri, mshambuliaji wa Yanga Prince Dube alifunga bao pekee la Zimbabwe katika mchezo huo na kuwa nyota wa kwanza kufunga miongoni mwa wachezaji wanaocheza ligi ya Tanzania.
Unaweza kusema Dube amezaliwa upya akiendeleza moto wake wa kuzifumania nyavu akifunga bao lake la nne katika mechi tano zilizopita.
Mapema jana Mali ililazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Zambia, mlinda lango Djigui Diarra akiwa langoni.
Leo timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' itashuka dimbani kuumana na Nigeria mchezo utakaopigwa saa 2:30 usiku
ADVERTISE HERE