Kuelekea dirisha dogo la usajili ambalo sasa litafunguliwa Januari 01, 2026, Meneja wa habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amethibitisha kuwa tayari mtendaji mkuu wa klabu hiyo Andre Mtine amepokea ripoti ya benchi la ufundi kuhusu mapendekezo ya maboresho yanayohitajika.
Kamwe amesema tayari uongozi umeanza kuifanyia kazi ripoti hiyo ambapo mazungumzo na wachezaji wanaohitajika yamefanyika.
"Ripoti imeshafika kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa klabu yetu na imeshaanza kufanyiwa kazi na tayari kwa asilimia 80 yote ambayo ripoti imeainisha kwa maana ya timu kuboreshwa tunakwenda nayovizuri."
"Tuko kwenye mazungumzo na wachezaji wasiopungua watatu na yanakwenda vizuri kwa asilimia 85"
"Tunaamini dirisha hili sio dirisha la kufanya bahati nasibu, ni dirisha la kwenda kuboresha maana tumefahamu ni maeneo gani tunahitaji kuongeza nguvu," alisema Kamwe.
Maeneo yanayotarajiwa kuboreshwa ni eneo la kiungo mkabaji, kiungo wa ushambuliaji na mshambuliaji