Boyeli mtegoni Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
18 Dec 2025
Boyeli mtegoni Yanga

Mshambuliaji wa Yanga Andy Boyeli ameanza majukumu yake na Wananchi kwa kusuasua na upo uwezekano akarejeshwa katika klabu yake ya Shekhukhune United ya Afrika Kusini, imefahamika.

Yanga ilimsajili Boyeli kwa mkopo wa msimu mzima ikiwa na matarajio makubwa kwake kuiongezea makali safu ya ushambuliaji ambayo msimu uliopita iliongozwa na Prince Dube, Clement Mzize na Kennedy Musonda.

Hata hivyo mpaka sasa ni kama mambo yamekwenda kinyume na matarajio akiwa na wakati mgumu kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza.

Boyeli amefunga mabao mawili kwenye ligi kuu ya NBC yote akiyafunga katika mchezo dhidi ya KMC.

Bado ameshindwa kulishawishi benchi la ufundi Yanga ikiendelea kumtegemea Mzimbabwe Prince Dube wakati huu ambao Mzize anaendelea kuimarika baada ya kufanyiwa upasuaji wa goti.

Tayari Yanga iko kwenye mchakato wa kusaka mshambuliaji mwingine wa kigenini hatua ambayo inaweka mashakani hatma ya Boyeli.

Mshambuliaji raia wa Angola Laurindo Dilson Maria Aureio 'Depu' anatajwa kuwa pendekezo la kocha Pedro Goncalves huku pia mabingwa hao wa soka Tanzania Bara kwa misimu minne mfululizo wakihusishwa kumuwania mshambuliaji wa Stade Malien Taddeus Nkeng Fomakwang raia wa Cameroon.

Dirisha dogo la usajili litafunguliwa Januari 1, 2026 na pengine mashabiki wa Yanga watarajie kuona sura mpya zikiingia eneo la ushambuliaji.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
7h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
11h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
16h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’