Uongozi wa Yanga uko kwenye hatua za mwisho kumalizana na kocha wa Kagera Sugar Meck Mexime ili awe kocha msaidizi kuchukua nafasi ya Shedrack Nsajigwa, imefahamika.
Taarifa za uhakika ni kwamba, Mexime kocha bora wa msimu wa 2016/17 amekubali kutua Yanga kusaidiana na Mwinyi Zahera ambaye ndiye kocha Mkuu.
Yanga ilijaribu kumpata Mexime bila mafanikio msimu uliopita wakati alipoondoka Juma Mwambusi lakini sasa inaelekea kufanikiwa wakati huu.
Mabadiliko ya benchi la ufundi la Yanga huenda yakamrejesha Shedrack Nsajigwa kwenye kikosi cha pili wakati Noel Mwandila akirejea kwenye majukumu yake ya kocha wa viungo.

ADVERTISE HERE