Baada ya kumkosa katika dirisha lililopita, klabu ya Mbeya City imepiga tena hodi mitaa ya Twiga na Jangwani kumtaka kiungo kiraka Faridi Mussa, imefahamika.
Farid amekuwa na wakati mgumu wa kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza msimu huu, Mbeya City wakimuhitaji kwa mkopo hadi mwishoni mwa msimu.
Upo uwezekano mkubwa Yanga ikiaridhia mkopo huo endapo Mbeya City watafikia makubaliano na mchezaji mwenyewe.
Katika hatua nyingine, TRA United nao wamepiga hodi Jangwani kumtaka winga Denis Nkane.

Licha ya kusaini mkataba mpya katika dirisha lililopita, Nkane bado ameshindwa kupenya katika kikosi cha kwanza.
Uongozi wa Yanga umeendelea kuwa na imani nae wakiamini muda wake utafika akiwa sehemu ya kikosi cha Yanga kwa takribani misimu minne sasa.
ADVERTISE HERE