Mshambuliaji wa Yanga Prince Dube amepenya katika kikosi cha Zimbabwe kinachokwenda kushiriki michuano ya Afcon 2025 inayotarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi huko Morocco.
Dube anatarajiwa kuwa silaha muhimu katika safu ya ushambuliaji ya Zimbabwe akiungana na washambuliaji wengine kama Bill Antonio na Washington Navaya.
Anaungana na nyota wengine watano wa Yanga ambao nao wamejumuishwa katika Mataifa yao kwa ajili ya michuano hiyo.
Mlinda lango Djigui Diarra yuko kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Mali wakati Mohammed Hussein, Ibrahim Bacca, Dickson Job na Bakari Mwamnyeto wakijumuishwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' ambacho tayari kimeingia kambini Misri.
ADVERTISE HERE