Katika ligi kuu ya NBC msimu huu, Yanga imeweka kambani mabao 12 huku ikiruhusu bao moja tu kutikisa nyavu zake.
Mapema tu Yanga inaongoza kuweka mipira kimiani, ikiwa sawa na JKT Tanzania ambayo hata hivyo imecheza mechi 10 huku Wananchi wakishuka dimbani mara 6 tu.
Prince Dube, Maxi Nzingeli, Andy Boyeli na Pacome Zouzoua ndio waliohusika kwenye mabao mengi, wakihusika katika mabao 8 kila mmoja akifunga mabao mawili.
Mabao mengine manne yamefungwa na Mudathir Yahya, Lassine Kouma, Mohamed Hussein na Celestin Ecua.
Upande wa vinara wa pasi za mabao, Duke Abuya anaongoza akitoa pasi tatu, akifuatiwa kwa karibu na Pacome Zouzoua aliyetoa asisti mbili.
Zimbwe Jr, Maxi, Ecua na Israel Mwenda kila mmoja ana pasi moja ya bao.
Katika mechi 6, Wananchi wameondoka na cleansheet 5 Djigui Diarra akiwa na tatu huku Aboutwalib Mshery akiwa nazo mbili