Goncalves anazitaka alama tatu Dodoma

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
6 Dec 2025
Goncalves anazitaka alama tatu Dodoma

Kocha Mkuu wa Yanga Pedro Goncalves amesema kikosi chake kiko tayari kwa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Coastal Union ambao utapigwa kesho Jumapili katika uwnja wa Jamhuri mkoani Dodoma.

Akizungumza katika mkutano na wanahabari mapema leo, Goncalves alisema licha ya kutopata muda wa kutosha kujiandaa na mchezo huo, anaamini katika ubora wa kikosi chake na vijana wake watakuwa tayari kuwania alama tatu katika mchezo huo mgumu.

"Maandalizi yetu siyo makubwa kuelekea mchezo wetu wa kesho kwasababu ya muda mchache tuliopata kutokea mchezo wetu uliopita, tuna baadhi ya Wachezaji wako sawa na kuna wengine wana uchovu. Lakini kwenye akili zetu tunajua ni nini tunataka na tuko hapa kutafuta alama 3"

"Namba za wapinzani wetu hazidanganyi, wameruhusu magoli machache kwenye michezo waliyocheza na kila mara tukikutana nao tunakuwa na mchezo mgumu, hata kesho tunajua hautakuwa mchezo mrahisi lakini tuna kikosi bora na tutapambana kuhakikisha tunaondoka na alama 3," alisema Goncalves

Akizungumza kwa niaba ya wachezaji wenzake, Offen Chikola amesema wachezaji wanafahamu umuhimu wa mchezo huo na watashuka uwanja wa Jamhuri hapo kesho kwa lengo la kutafuta alama tatu.

"Kwa niaba ya wachezaji wenzangu tumejiandaa vizuri kuwakabili Coastal Union kesho, ni kweli mechi zetu huwa zinakuwa na ugumu lakini tunajua umuhimu wa mchezo wa kesho na tumejiandaa kuondoka na ushindi"

"Wanachama na Mashabiki wetu ni sehemu muhimu kwenye timu yetu, Dodoma ni nyumbani na tunaamini kesho watajitokeza kwa wingi kuja kutupa sapoti," alisema Chikola

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
4h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
4h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
4h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
8h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
23h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
23h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’