Yanga 'kumtuza' Diarra KMC Complex

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
2 Dec 2025
Yanga 'kumtuza' Diarra KMC Complex

Alhamisi Disemba 04 uwanja wa KMC Complex Yanga itarejesha makali yake kwenye ligi kuu ya NBC pale watakapoikaribisha Fountain Gate katika moja ya mechi za viporo ambazo Wananchi wanatarajiwa kucheza kabla ya ligi kusimama kwa zaidi ya mwezi mmoja kupisha michuano ya Afcon 2025.

Baada ya mchezo huo Yanga itarudi tena dimbani Disemba 07 kuumana na Coastal Union katika mchezo ambao mpaka sasa bado haijafahamika utapigwa wapi kwa kuwa dimba la Mkwakwani limefungiwa, wenyeji Coastal Union wakitarajiwa kuchagua uwanja mwingine.

Kuelekea mchezo dhidi ya Fountain Gate, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amesema mchezo huo utakuwa maalum kumpongeza mlinda lango Djigui Diarra baada ya kazi nzuri aliyofanya kule Algeria katika mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya JS Kabylie.

Diarra alionyesha ushujaa wa aina yake katika mchezo huo kwani alipata majeraha kwenye kipindi cha kwanza lakini alirejea uwanjani kwenye kipindi cha pili akiwa na maumivu na kufanya 'save' za maana ambazo kwa kiasi kikubwa zilichangia Yanga kuondoka na alama moja muhimu ugenini.

Kamwe amesema Alhamisi itakuwa siku ya Diarra 'kuokota' kutoka kwa mashabiki, utaratibu ambao mashabiki wa Yanga wameubuni kuwatuza wachezaji wao kila wanapocheza dimba la nyumbani.

"Nawaalika mashabiki wa Yanga waje kwa wingi Alhamisi dimba la KMC Complex kwenye mchezo wetu dhidi ya Fountain Gate"

"Njooni tuiunge mkono timu yetu katika mchezo huu lakini pia tuwapongeze wachezaji wetu na kipekee tumpe shukrani golikipa wetu Djigui Diarra"

"Siku hiyo Diarra hatatumia begi, tutamkabidhi 'shangazi kaja' na Wananchi tuhakikishe linajaa," alisema Kamwe

Diarra amekuwa kwenye kiwango bora tangu kuanza kwa msimu huu akicheza mechi zote za mashindano

Hata hivyo majeraha aliyopata Algeria huenda yakamfanya akose mchezo dhidi ya Fountain Gate nafasi yake ikitarajiwa kuchukuliwa na Aboutwalib Mshery au Aboubakar Khomein

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
13h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’