Yanga yalalamika kufanyiwa vurugu Algeria

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
1 Dec 2025
Yanga yalalamika kufanyiwa vurugu Algeria

Klabu ya Yanga imewasilisha malalamiko kwa Shirikisho la mpira barani Afrika (CAF) kufuatia matukio yaliyojitokeza kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya JS Kabylie uliopigwa Algeria siku ya Ijumaa na kumalizika kwa matokeo ya suluhu ya bila kufungana.

Wakati mchezo huo ukiendelea mashabiki wa JSK walionekana mara kwa mara wakimshambulia mlinda lango wa Yanga Djigui Diarra kwa kumrushia mawe na makopo ya maji.

Matukio hayo yalishamiri kwenye kipindi cha pili hadi kupelekea mchezo huo kusimama kwa dakika kadhaa na kisha kuendelea tena baada ya utulivu kurejea.

Hata hivyo baada ya mchezo kumalizika, mashambulizi zaidi yakapelekwa kwa wachezaji, benchi la ufundi wakati wakitoka uwanjani.

Menaja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amethibitisha kuwa Yanga imewasilisha malalamiko yao, hivyo wameiachia CAF kuamua.

"Kwanza tunashukuru kwa kurejea salama kutoka Algeria. Hatukuweza kutimiza malengo yetu kwa asilimia 100 lakini tunashukuru tumerejea nyumbani na alama 1"

"Mazingira ya mchezo dhidi ya JS Kabylie yalikuwa magumu, tulikutana na changamoto tangu siku tumewasilia Algeria na hata baada ya mchezo"

"Tumewasilisha malalamiko ya matukio tuliyofanyiwa kwa msimamizi wa mchezo na uzuri hata maafisa wa usalama wa CAF walikuwepo uwanjani na walishuhudia kila kitu"

"Msimamizi wa mchezo ametuhakikishia wamechukua malalamiko yetu na yatafanyiwa kazi. Hatulalamiki ili JS Kabylie waadhibiwe, CAF wenyewe wanajua hatua gani za kuchukua kwa kuzingatia kanuni zao"

"Tunachotaka sisi ni kukomeshwa kwa matukio haya yanayofanywa na wenzetu tunapokwenda kucheza katika nchi zao, alisema Kamwe"

Hii sio mara ya kwanza kwa Yanga kukumbana nna vurugu za mashabiki nchini Algeria. Mwaka 2023 walipokuwa nchini humo kucheza fainali ya kombe la Shirikisho (CAFCC) dhidi ya USM Alger, matukio ya aina hiyo yalijitokeza.

Yanga ilishambuliwa kuanzia hoteli waliyofikia, uwanja wa July 05 uliochezwa mchezo huo wa fainali ulikuwa kama eneo la vita. Fataki mfululizo na matukio ya kusimamisha mchezo kila mara.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
1h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
1h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
5h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
20h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
20h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’