Sasa waseme kundi la kifo ni lipi?

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
1 Dec 2025
Sasa waseme kundi la kifo ni lipi?

Wakati CAF walipofanya droo ya makundi CAFCL Yanga ilipotangazwa kuwa kundi moja na timu za Al Ahly, AS FAR na JS Kabylie, maoni ya kuisikitikia Yanga yalikuwa mengi.

Baadhi ya wachambuzi waliibeza Yanga wakiamini haitakuwa na nafasi katika kundi hilo D mbele ya timu kutoka Kaskazini mwa Afrika ambazo zote zina historia ya kutwa taji la ligi ya mabingwa.

Lakini baada ya kukamilika kwa mechi mbili, lugha zimeanza kubadilika Yanga ikianza vyema kampeni yake ya kuisaka tiketi ya robo fainali katika kundi hilo la kifo.

Wananchi wanashika nafasi ya pili wakiwa na alama nne sawa na Al Ahly inayoongoza kwa tofauti ya uwiano wa mabao.

Mabingwa hao wa soka Tanzania Bara wamewafunga midomo wale waliokuwa 'wakiwabeza' kwani mpaka sasa ndio timu pekee inayopeperusha vyema bendera ya Tanzania katika mashindano ya CAF msimu huu.

Yanga ndio timu pekee ambayo haijapoteza mchezo huku watani zao Simba waliokuwa wakipambwa kwa kila aina ya sifa wamepoteza mechi zote mbili kama ilivyo kwa Azam Fc iliyoanza vibaya kampeni yao kwenye kombe la Shirikisho.

Singida BS angalau jana iligoma kufungwa nyumbani ikipata sare ya bao 1-1 dhidi ya Stellenbosch ya Afrika Kusini.

Mpaka sasa unaweza kusema Yanga imejibu kejeli na dharau uwanjani, Wananchi waliwaacha wakosoaji wao wamalize maneno na sasa wamewafunga midomo...!

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
5h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
9h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
14h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
14h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
17h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’