Baada ya ligi kumalizika jana, dirisha la usajili linatarajiwa kufunguliwa wakati wowote huku baadhi ya timu zikiwa zimeanza usajili mapema kwa kasi.
Simba tayari imekamilisha usajiliwa wachezaji wawili Adam Salamba na Marcel Kaheza ambao wote walikuwa pia wakiwaniwa na Yanga.
Kuna taarifa kuwa Simba pia iko mbioni kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa Prisons, Mohammed Rashidi.
Viongozi wa Yanga nao inatakiwa washituke, waanze kufanya mambo 'chapchap' kwani usajili wa msimu huu upinzani hautoki kwa Simba pekee, kuna Azam FC bila kuisahau Singida United.
Hakuna ubishi kwamba kikosi cha Yanga kinahitaji marekebisho makubwa ili kuweza kuleta ushindani kwenye ligi msimu ujao.
Yanga inahitaji mchanganyiko wa wachezaji chipukizi na wazoefu.
Ni jambo jema kwa Kamati ya usajili inayoongozwa na Hussein Nyika kuachana na mpango wa kujaribu wachezaji ili wasajiliwe.
Yanga ni lazima isajili wachezaji ambao ina uhakika na viwango vyao, utaratibu wa 'scouting' unaopendekezwa na wengi ndio unaofaa kufuatwa.

ADVERTISE HERE