Baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya AS FAR jana, kikosi cha Yanga kimerejea jijini Dar es salaam tayari kwa safari ya kuelekea Algeria.
Meneja wa Yanga Walter Harrison amesema timu itaondoka jijini Dar es salaam kesho Jumatatu, Novemba 24 majira ya saa 9 mchana kuelekea Algeria.
Mchezo dhidi ya JS Kabylie utapigwa Ijumaa, Novemba 28 saa 4 usiku kwa saa za Tanzania.
Wakati Yanga ikishinda dhidi ya AS FAR, wapinzani wao Kabylie walikutana na kipigo cha mabao 4-1 kutoka kwa Al Ahly huko Misri.
Baada ya mechi za raundi ya kwanza kukamilika, Al Ahly wako kileleni na alama 3 sawa na Yanga inayoshika nafasi ya pili Ahly wakifunga mabao mengi zaidi
ADVERTISE HERE