Job awaita mashabiki New Amaan Complex

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
21 Nov 2025
Job awaita mashabiki New Amaan Complex

Nahodha Msaidizi wa Yanga Dickson Job amesema uwanja wa New Amaan Complex hauna ugeni kwao kwani wamecheza mechi kadhaa za mashindano katika uwanja huo na hivyo wako tayari kukabiliana na AS FAR katika mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi CAFCL katika uwanja huo.

Job amesema maandalizi ya mchezo huo yamekamilika huku akiwataka mashabiki kujitokeza kwa wingi dimba Amaan ili kuwaongezea hamasa.

"Kwa niaba ya Wachezaji wenzangu tumejipanga vyema sana. Tupo tayari kukabiliana na kila mpinzani ambaye anakuja mbele yetu. Tuna imani na matarajio makubwa kuhakikisha kuwa tunapata alama tatu muhimu kesho."

"Tumekuwa na mechi kadhaa za Kimataifa ambazo tumecheza katika Uwanja huu wa Amaan. Wana Yanga wamejaa kila kona ya nchi yetu kila tunapoenda lazima tupate hamasa ya kutosha kwa mashabiki na tuna imani kwa hamasa yao kesho itatusaidia kufanya vizuri uwanjani," alisema Job

Yanga leo inatarajiwa kukamilisha maandalizi yake ya mwisho katika dimba la Amaan tayari kwa mtangange dhidi ya AS FAR utakaopigwa kesho Jumamosi, saa 10 jioni katika uwanja huo

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
2h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
7h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
8h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
8h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
11h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’