Yanga yajipanga kwa maboresho muhimu dirisha dogo

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
17 Nov 2025
Yanga yajipanga kwa maboresho muhimu dirisha dogo

Ni uhakika mlinzi wa kulia Yao Kouassi yuko tayari kurejea kikosini baada ya kupona majeraha na kuanza mazoezi ya timu kikamilifu.

Yao hajaonekana uwanjani tangu mwezi April mwaka huu alipopata changamoto ya goti iliyomfanya afanyiwe upasuaji ambao umemuweka nje kwa takribani miezi sita.

Hatua hiyo pia ilipelekea uongozi wa Yanga kutomjumuisha katika miongoni mwa wachezaji wake waliosajiliwa kushiriki mashindano mbalimbali.

Hata hivyo baada ya kupona sasa anahesabu siku tu kwani ifikapo Disemba 15 Yanga inaweza kumrejesha katika kikosi kupitia dirisha dogo.

Mbali na eneo la safu ya ulinzi, kulingana na afisa mmoja wa benchi la ufundi, Yanga pia huenda ikaongeza nguvu eneo la safu ya ushambuliaji ambalo kwa sasa linaongozwa na Prince Dube na Andy Boyeli wakati Clement Mzize akiwa bado majeruhi.

Dube ameanza kwa kusuasua msimu huu huku Boyeli 'akiwaka' katika mchezo uliopita wa ligi baada ya kufunga mabao mawili, bado ufanisi wa eneo hilo hauridhishi.

Tetesi zinaihusisha Yanga na mshambuliaji wa Stade Malien,Taddeus Nkeng Fomakwang kuwa anaweza kutua kwa Wananchi pale dirisha dogo litakapofunguliwa.

Eneo la kiungo mkabaji nalo linatajwa kuhitaji maboresho hasa baada ya Moussa Balla Conte kushiindwa kufikia matarajio.

Kwa sasa Yanga inalazimika kumtumia Duke Abuya katika eneo hilo akishirikiana na Aziz Andabwile ambaye alianza vyema msimu kabla ya kupoteza nafasi yake baada ya kocha Romain Folz kupewa mkono wa kwaheri nafasi yake ikichukuliwa na Pedro Goncalves.

Yanga inalazimika kurudi sokoni kumsaka mbadala wa Khalid Aucho ambaye alijiunga na Singida BS baada ya kushindwa kufikia makubaliano ya kimkataba kati yake ya Yanga.

Safu ya kiungo mshambuliaji nayo inaweza kuongezewa nguvu, eneo ambalo kwa sasa anategemewa zaidi Mohamed Doumbia.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
6h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
10h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
15h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
15h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’