Ligi Kuu ya Wanawake (WPL) imeanza kutimua vumbi leo ambapo Yanga Princess ilianzia ugenini Ruangwa mkoani Lindi dhidi ya Ruangwa Queens.
Dakika 90 za mchezo huo zimemalizika kwa Yanga Princess kuibuka na ushindi wa mabao 3-0.
Mabao ya Yanga Princess katika mchezo huo yalifungwa na Precious Christopher aliyeweka kambani mabao mawili huku Aregash Tadese akiweka kambani bao jingine.
Ni mwanzo mzuri kwa kocha Edna Lema ambaye msimu huu ameandaa kikosi cha kuwania ubingwa.

ADVERTISE HERE