Yanga kumaliza msimu kwa kishindo?

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
28 May 2018
Yanga kumaliza msimu kwa kishindo?
Leo ligi kuu ya Vodacom inafika tamati kwa mabingwa wa msimu uliopita, Yanga kuikabili Azam FC kwenye mchezo wa mwisho utakaopigwa kwenye uwanja wa Taifa.

Wakati michezo mingine saba ikitarajiwa kuanza muda mmoja (saa 10) ili kuepuka kupanga matokeo, mchezo wa Yanga dhidi ya Azam FC utaanza saa mbili usiku.

Msimu huu haukuwa mzuri sana kwa Yanga kutokana na kukumbwa na changamoto nyingi za nje na ndani ya uwanja, lakini leo ina nafasi ya kumaliza msimu kwa kishindo kama itaweza kuifunga Azam FC na kushika nafasi ya pili.

Ikiwa na alama 52, Yanga inahitaji ushindi wa aina yoyote kuweza kuiondosha Azam Fc kwenye nafasi ya pili.

Ushindani baina ya timu hizo umekuwa ukiongezeka siku hadi siku.

Juzi Azam FC imemsajili aliyekuwa mshambuliaji wa Yanga Donald Ngoma na kuna taarifa kuwa imepania kuwasajili wachezaji wengine wawili (Yondani na Abdul) ambao mikataba yao imemalizika.

Miaka mitatu nyuma Azam FC pia iliwasajili Frank Domayo na Didier Kavumbagu kabla ya Yanga kujibu mapigo msimu uliopita kwa kumsajili Gadiel Michael.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
9h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
13h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
18h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
18h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’