Kiungo mshambuliaji wa Yanga Pacome Zouzoua jana aliondoka na tuzo ya nyota wa mchezo akiiongoza Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya KMC katika mchezo uliopigwa uwanja wa KMC Complex.
Pacome alifunga moja ya mabao hayo huku pia akitoa pasi ya bao la kwanza lililofungwa na Maxi Nzengeli.
Hiyo ni tuzo yake ya kwanza ya nyota wa mchezo msimu huu akianza safari ya kuvunja rekodi ya tuzo nane alizobeba msimu uliopita.
Wakati tuzo za TFF za msimu uliopita zikitarajiwa kutolewa mwezi Disemba, Pacome anatarajiwa kuondoka na tuzo ya MVP baada ya kuisaidia Yanga kutetea taji la ligi kuu kwa msimu wa nne mfululizo



ADVERTISE HERE