Unaweza kusema mlinda lango wa Yanga Djigui Diarra 'hacheki na wowote' msimu huu kwani amepania kurejea ufalme wake katika ligi kuu ya NBC.
Baada ya kukosa tuzo ya mlinda lango bora kwa misimu miwili iliyopita, Diarra amerejea akiwa na dhamira ya kuibeba tuzo hiyo.
Mpaka sasa hajaruhusu bao katika lango lake kwenye ligi katika mechi tatu alizokaa mbele ya milingoti.
Aidha amekuwa mlinda lango wa kwanza kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi ligi kuu ya NBC, akitwaa tuzo hiyo mwezi uliopita.
Katika mechi nne za hatua ya awali ligi ya mabingwa, Diarra aliruhusu bao moja likiwa ndio goli pekee alilofungwa katika mashindano yote msimu huu.


ADVERTISE HERE