Kikosi cha Yanga Jumapili Novemba 09 kitakuwa dimbani KMC Complex kuwakabili KMC katika mwendelezo wa ligi kuu ya NBC.
Huu utakuwa mchezo wa pili kwa Yanga kushuka dimba la KMC Complex msimu huu baada ya ushindi wa mabao 2-0 katika mchezo uliopita dhidi ya Mtibwa Sugar.
Yanga ilirejea mazoezini juzi chini ya Kocha Mkuu Pedro Goncalves ambaye sasa amepata muda zaidi wa kufanya mazoezi na kikosi chake tangu alipotua Oktoba 25.
Baada ya kumalizana na Mtibwa Sugar, mipango itaelekezwa kwenye ligi ya mabingwa mechi za hatua ya makundi zikitarajiwa kuanza kutimua vumbi mwishoni mwa mwezi huu.
Yanga itaanzia nyumbani dhidi ya AS FAR na kisha kusafiri Algeria kuikabili JS Kabylie.
ADVERTISE HERE