Yanga imejipanga 'kutoboa' kundi la kifo

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
6 Nov 2025
Yanga imejipanga 'kutoboa' kundi la kifo

Licha ya kukiri kuwa Yanga itakabiliwa na upinzani mkali katika kusaka tiketi ya kutinga robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika (CAFCL), Meneja wa habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amewataka mashabiki na wanachama kuwa tayari kuiunga mkono timu yao katika kila mechi na kipekee zaidi zile zitakazochezwa uwanja wa nyumbani.

Jana Yanga ilitangaza uamuzi wake wa kucheza mechi tatu za nyumbani katika uwanja wa New Amaan Complex visiwani Zanzibar.

Kamwe amesema Yanga iko katika kundi gumu linalojumuisha timu nne kutoka ligi tano bora barani Afrika.

Ni kundi B linalozijumuisha Al Ahly kutoka Misri ambapo ligi ya nchini humo inatajwa kuwa namba moja, AS FAR ya Morocco ligi ya nchi hiyo ikishika nafasi ya pili kwa ubora ikifuatiwa na ligi ya Algeria nafasi ya tatu inakotoka klabu ya JS Kabylie na Yanga ya Tanzania ligi kuu ikishika nafasi ya tano.

"Ni kundi Gumu. Kundi la kifo. Kundi lililobeba ukubwa wa mpira wa Afrika. Ligi 5 kwa ubora na ugumu Afrika, zimekusanywa kwenye kapu moja. Ni vita hii. Fahari na heshima vitapatikana kwa pamoja katika kila dakika 90 za mechi zake."

"Hili ni Kundi la kuliendea kwa Utulivu na umakini mkubwa. Ni Kundi la mawindo na mitego mingi. Hutakiwi kufunga jicho.Tuna nafasi ya kufuzu hapa kuelekea Robo Fainali. Tulishawahi kuwa kwenye nyakati kama hizi na tukafanya makubwa zaidi"

"Tuanze maandalizi Wananchi Visiwa vya Unguja na Pemba vikawe machinjio ya Waarabu. Tukaandae sumu ya maangamizi. We are Young Africans Sports Club na haikuwa bahati mbaya, Tuliposema, DAIMA MBELE NYUMA MWIKO"

"Baadhi wameshatukatia Tamaa, tumewasikia kwa uzuri kabisa. Ombi langu kwenu Wananchi, kwa sasa tusijibishane nao kwa midomo, vitendo vitazungumza. Tujiweke tayari," alisema Kamwe

Yanga itaanza kampeni yake ya kuisaka robo fainali dhidi ya AS FAR Novemba 21-23 hapo katika dimba la New Amaan Complex

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
26m ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
5h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
5h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
15h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
18h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
23h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’