Gumbo awatoa hofu Wanayanga makundi CAFCL

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
5 Nov 2025
Gumbo awatoa hofu Wanayanga makundi CAFCL

Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Yanga, Rodgers Gumbo amewahakikishia Wanachama na Mashabiki wa timu hiyo kuwa wamejipanga kufanya vyema hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika.

Droo ya makundi ya michuano hiyo ilifanyika juzi Afrika Kusini ambapo Yanga imepangwa kundi B pamoja na klabu za Al Ahly, AS FAR na JS Kabylie.

Baadhi ya mashabiki wa Yanga ni kama wameingiwa hofu juu ya timu yao kufanya vyema katika kundi hilo ambalo wengi wanalitazama kama kundi la kifo Yanga ikiwa dhidi ya timu tatu kutoka Afrika ya Kaskazini

Gumbo amesema Wanayanga hawana sababu ya kuihofia timu yoyote zaidi ya kutakiwa kuwaheshimu kwa kiasi wapinzani na kwamba watakuwa na hesabu za kimyakimya na zile za hadharani namna ya kwenda kuzicheza mechi hizo.

"Unaweza kusema ni kundi gumu lakini sisi ni Yanga tunajua ubora wa wapinzani wetu lakini tutajipanga kukabiliana na timu moja kwenda nyingine bila unyonge."

"Tuna timu imara sana na hivi karibuni mmeona tumeboresha benchi letu la ufundi kwa kumleta kocha mkubwa, tuko kwenye afya nzuri ya kwenda kushindana."

"Tunakwenda kujipanga sawasawa, tutakutana na benchi la ufundi lakini yapo mambo yatakuwa hadharani na mambo mengine hayatakuwa wazi, sio kila taarifa ya kukabiliana na adui yako inatakiwa kufika kwa mpinzani.

"Mashabiki wetu hawatakiwi kutishwa, Yanga ni kubwa, wanaodhani tutaanguka, tunatakiwa kwenda kuwathibitishia kwa vitendo ukubwa wetu, kuna ratiba huko nyuma zilitoka tukaona tutashinda lakini tukakwama na kuna ratiba pia tuliziona ngumu baadaye tukatoboa," alisema Gumbo

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
7h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
10h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
15h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’