Ratiba kamili ya mechi za hatua ya makundi ligi ya mabingwa barani Afrika imewekwa hadharani na shirikisho la soka barani Afrika (CAF) ambapo mabingwa wa soka Tanzania Bara Yanga wana mtihani kundi B kusaka tiketi ya kufuzu robo fainali mbele ya Al Ahly, AS FAR na JS Kabylie
Habari njema kwa mashabiki wa Yanga ni kuwa timu yao itaanzia kampeni ya kufuzu robo fainali uwanja wa nyumbani dhidi ya AS FAR itahitimisha kampeni hiyo nyumbani dhidi ya JS Kabylie.
Mechi ya kwanza ni Novemba 21-23 2025 na mechi ya mwisho ni Februari 13-15 2026 dimba la Benjamin Mkapa.
Mechi mbili tu zitapigwa mwishoni mwa mwezi huu, michuano hiyo itasimama kwa miezi miwili kupisha mechi za kalenda ya FIFA na CAF
Mechi nne za kuhitimisha makundi zitapigwa kuanzia mwishoni mwa Januari 2026 na kutakuwa na takribani wiki nne za bandika bandua
Kwa kuzingatia ratiba, kama Wananchi watachanga vyema karata zao, unaona kabisa nafasi ya kutinga robo fainali ni kubwa na iko mikononi
Ratiba ya mechi zote;
- Nov 21-23 - Yanga vs AS FAR
- Nov 28-30 - JS Kabylie vs Yanga
- Jan 23-25 - Al Ahly vs Yanga
- Jan 30-Feb 1 - Yanga vs Al Ahly
- Feb 06-08 - AS FAR vs Yanga
- Feb 13-15 - Yanga vs JS Kabylie