Ligi Kuu ya Vodacom msimu wa 2017/18 inamalizika leo Jumatatu, May 28 2018 kwa timu zote 16 kuteremka dimbani.
Ligi hiyo iliyoanza August 26 2017 imeishuhudia Simba ikitawazwa kuwa mabingwa wapya wakati Njombe Mji ikiwa timu ya kwanza kujihakikishia kuteremka daraja msimu huu.
Matokeo ya michezo kati ya Majimaji dhidi ya Simba na Ndanda Fc dhidi ya Stand United yataweza kubainisha timu ya pili itakayoteremka daraja.
Majimaji ni lazima iifunge Simba huku pia ikiomba Ndanda FC ipoteze mchezo wake.
Ndanda huenda ikahitaji alama moja tu kujinusu kuteremka daraja kama Majimaji itashindwa kuifunga Simba zaidi ya mabao matatu.
Michezo ya kumaliza msimu

Wakati michezo mingine ikitarajiwa kupigwa saa kumi jioni, mchezo wa Yanga dhidi ya Azam FC utapigwa kwenye uwanja wa Taifa saa mbili usiku.
Mchezo huo pia utabainisha timu itakayomaliza kwenye nafasi ya pili, Yanga ikihitaji ushindi wakati Azam ikihitaji sare tu.

ADVERTISE HERE