Matumaini ya mashabiki wa Yanga kumshuhudia mshambuliaji Clement Mzize katika mchezo uliopita wa ligi ya mabingwa dhidi ya Silver Strikers yalifutika baada ya mshambuliaji huyo kupata majeraha siku moja kabla ya mchezo
Licha ya kumkosa nyota huyo, Yanga ilifanikiwa kutinga hatua ya makundi baada ya ushindi wa mabao 2-0 yaliyofungwa na Dickson Job na Pacome Zouzoua
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amethibitisha kuwa Mzize alitonesha majeraha na sasa atafanyiwa tena vipimo kubaini changamoto inayomkabili
“Clement Mzize anakwenda kufanyia vipimo vingine ili kubaini ukubwa wa jeraha lake. Mzize alijitonesha kwa bahati mbaya alipokuwa mazoezini. Mpaka hapo baadae madaktari wetu watatupatia ripoti kamili,” alisema Kamwe
Katika hatua nyingine Kamwe ametangaza safu ya benchi la ufundi la Yanga ambapo amesema kocha Pedro Goncalves ndiye atakayeongoza benchi hilo akisaidiwa na makocha wasaidizi wawili Philipe Pedro na Patrick Mabedi