Jana ilikuwa siku nyingine mbaya ofisini kwa mshambuliaji Prince Dube ambaye jambo pekee ambalo unaweza kusema kwa sasa ni kuwa anapita katika kipindi kigumu.
Ni kama alivyoanza msimu uliopita, amepoteza makali yake mbele ya lango licha ya juhudi zake kubwa uwanjani.
Kocha Patrick Mabedi alimuamini na aliendelea kumuacha uwanjani hata pale ilipoonekana anapoteza nafasi nyingi
Lakini baadae ni Dube mwenyewe aliyeomba kufanyiwa 'sub' baada ya kuona jitihada zake zinakwama
Benchi la ufundi limeendelea kuwa na imani na Dube kuongoza safu ya ushambuliaji ya Yanga kwa sababu nyota huyo wa Kimataifa wa Zimbabwe anafanya vyema katika uwanja wa mazoezi
Ni nyakati ngumu tu Mwana Mfalme anapitia lakini bila shaka atarejea katika ubora wake
ADVERTISE HERE