Lilikuwa ni suala la muda, Petro Goncalves raia wa Ureno ametambulishwa kuwa kocha mkuu wa Yanga akichukua mikoba iliyoachwa na Romain Folz
Uongozi wa Yanga ulilazimika kusubiri dakika 90 za mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Silver Strikers zikamilike Yanga ikitinga hatua ya makundi baada ya ushindi wa mabao 2-0
Goncalves alitua Dar mapema majira ya mchana na alikuwepo dimba la Mkapa kushuhudia mchezo huo
Jukumu lake la kwanza ni kuhakikisha anarejesha soka burudani la Wananchi ambalo mashabiki wengi wa.Yanga wanaamini lilikuwa mashakani chini ya Folz
Karibu Jangwani Goncalves
ADVERTISE HERE