Wachezaji wako tayari kuikabili Silver Strikers - Mabedi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
24 Oct 2025
Wachezaji wako tayari kuikabili Silver Strikers - Mabedi

Kaimu kocha Mkuu wa Yanga Patrick Mabedi amesema wachezaji wake wako tayari kwa mchezo wa mkondo wa pili kuwania tiketi ya kutinga hatua ya makundi ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya Silver Strikers ya Malawi.

Kesho Jumamosi, saa 11 jioni Yanga itakuwa mwenyeji wa Silver Strikers katika mchezo utakaopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa huku Yanga ikihitaji aina moja tu ya matokeo, ushindi utakaotosha kufuzu hatua ya makundi.

Akizungumza katika mkutano na wanahabari mapema leo akiweka bayana maandalizi ya mchezo huo, Mabedi alisema wamepata muda wa kujiandaa, ari na morali ya wachezaji wake iko juu akiwa na matarajio makubwa kuelekea mchezo huo.

Mabedi amesema anatambua kuna presha kubwa nyuma ya mchezo huo lakini yeye kama kocha ni kazi yake kupambana na mazingira hayo lengo likiwa kuishinda presha hiyo

"Tulianza kambi yetu Jumanne baada ya mchezo wetu wa kwanza dhidi ya Silver Strikers, Malawi. Wachezaji wamejiandaa vizuri na kuna nguvu kubwa, hamasa na ari baina yao kuelekea mchezo huu muhimu wa kesho"

"Kwenye mpira kila mchezo una presha na sisi tunaishi kwenye hiyo presha na tunajua kuna presha kubwa hasa kwa mashabiki wetu lakini jambo la muhimu kwenye mchezo wa kesho nikufanya vizuri na kusonga mbele ili kuondoa hiyo presha na Wachezaji wote wamejiandaa vizuri na wako tayari kuipambannia nembo ya Klabu yetu”

"Kesho tunatakiwa kushambulia tu hatutakiwi kukaa nyuma. Tayari wapinzani wetu wako mbele kwa goli moja na tunatakiwa kuhakikisha tunashinda mchezo wa kesho ili tusonge mbele na huo ndo ukweli na wala hakuna njia nyingine," alisema Mabedi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
4h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
4h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
8h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
13h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
13h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
23h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’