Timu ya Silver Strikers kutoka Malawi, inatarajiwa kuwasili nchini leo Alhamisi kuelekea mchezo wa mkondo wa pili kuwania tiketi ya kutinga hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya Yanga
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amesema timu hiyo itatua nchini majira ya saa 2:30 usiku
Aidha Kamwe amesema Silver Strikers watapata nafasi ya kufanya mazoezi katika uwanja wa Benjamin Mkapa siku ya kesho Ijumaa saa 11 muda wa mchezo utakaopigwa Jumamosi
Kwa upande wa Yanga inaendelea na maandalizi yake kuelekea mchezo huo ambao Wananchi wanahitaji matokeo ya aina moja tu, ushindi wa angalau mabao 2-0 ili kufuzu robo fainali
Kocha wa muda Patrick Mabedi amepania kupindua meza na kuipeleka Yanga hatua ya makundi
ADVERTISE HERE