Hatma ya kufuzu iko mikononi mwetu - Kamwe

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
22 Oct 2025
Hatma ya kufuzu iko mikononi mwetu - Kamwe

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amesema hatma ya kufuzu hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa mbele ya Silver Strikers iko mikononi mwa Wananchi wenyewe.

Jumamosi Oktoba 25 Yanga itakuwa mwenyeji wa Silver Strikers katika mchezo wa marudiano utakaopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa baada ya kupoteza mchezo wa mkondo wa kwanza kwa bao 1-0 ambao ulipigwa nchini Malawi.

Kamwe amesema wachezaji wako tayari kwa asilimia 100 na jukumu la mashabiki ni kuhakikisha wanajitokeza kwa wingi kujaza dimba la Mkapa ili kuwaongezea ari na hamasa.

Kamwe amesema kama wachezaji watajitoa kwa asilimia 100, Yanga itashinda na kusonga mbele hatua ya makundi.

"Kuelekea mchezo dhidi ya Silver Strikers, ari na morali ya wachezaji ndio silaha yetu pale uwanja wa Benjamin Mkapa na niwaambie tu wachezaji wako tayari kwa asilimia 100."

"Kama Duke Abuya ataamua leo naenda kufuzu, Mudathir, Maxi na Pacome wakiamua, huyo Uchizi hamtamsikia na hamtamzungumza hata kwa dakika moja," alitamba Kamwe

Yanga iliingia kambini jana kwa ajili ya maandalizi ya mchezo huo chini ya Kaimu kocha Mkuu Patrick Mabedi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
7h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
11h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
16h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’