Kikosi cha Yanga kimerejea salama kutoka Malawi ambako walikamilisha mchezo wa mkondo wa kwanza kuwania tiketi ya kutinga hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya Silver Strikers
Wananchi walitua Dar jana usiku ambapo leo wachezaji wanaingia kambini Avic Town kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa mkondo wa pili utakaopigwa Jumamosi, Oktoba 25 uwanja wa Benjamin Mkapa
Tayari Yanga imetangaza viingilio vya mchezo huo hamasa kubwa ikitarajiwa kufanyika ili kuhakikisha Wananchi wanajitokeza kwa wingi kujaza dimba la Mkapa
Hii ni mechi ya kwenda makundi, Yanga ikihitaji angalau ushindi wa mabao 2-0 ili kufanikisha dhamira hiyo
ADVERTISE HERE