Klabu ya Yanga leo imeweka rekodi kwa kuzindua matawi matatu ya Wanachama nchini Malawi
Hafla ya uzinduzi wa matawi hayo ilifanyika mapema leo, Rais wa Yanga Injinia Hersi Said akifanya uzinduzi huo wa kihistoria
Akizungumza katika hafla hiyo, Hersi alimpongeza Mkurugenzi wa Mashabiki na Wanachama Ibrahim Samwel kwa jitihada za kuiweka Yanga karibu na wadau wake ndani na nje ya nchi
Hersi amewataka Wanachama walipie ada zao kwa wakati ili kuhakikisha wanakuwa sehemu ya maendeleo ya klabu yao
"Niwapongeze sana idara ya Wanachama na mkurugenzi wake Ibrahim Samwel kwa kazi kubwa ambayo wanafanya. Kazi yao kubwa ambayo imefana ni ubora wa mahusiano ya Klabu na Wanachama. Leo hapa Malawi tunaweka rekodi ya kufungua matawi matatu ya Klabu yetu"
"Historia ya Yanga na Malawi ni ndefu na imejenga heshima kubwa kwa Klabu yetu na kuimarisha mahusiano yetu kama Klabu na Taifa hili. Hapo baadae kwa kutambua mchango mkubwa wa Kocha Jack Chamangwana, tumemwalika Mke wake awe mmoja wa wageni wetu maalum kwenye mchezo wa leo."
"Itakuwa heshima kubwa kwetu ikiwa katika benchi letu la ufundi pia atakuwepo Kocha Mabedi ambaye ni Raia wa Malawi. Historia ya Mabedi haipishani sana na historia ya Kocha Chamangwana. Pasina shaka naye ataweka alama kubwa ya mafanikio kwa Klabu yetu"
"Niwaombe sana Viongozi wa Matawi kuendelea kuhamasisha Wanachama wetu kulipa ada zao. Kama ulishalipa ada na muda umekwisha basi ni vyema kuhakikisha kuwa unatimiza wajibu wako wa kikatiba kwa nia ya kusaidia uchumi wa Klabu hii. Asanteni sana wanachama wetu wapya wa Malawi kwa kuonesha nia njema ya kuichangia Klabu yao," alisema Hersi