Tumejiandaa kimkakati kuikabili Silver Strikers - Folz

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
17 Oct 2025
Tumejiandaa kimkakati kuikabili Silver Strikers - Folz

Kocha Mkuu wa Yanga Romain Folz amesema maandalizi kuelekea mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Silver Strikers utakaopigwa kesho Jumamosi katika uwanja wa Bingu yamekamilika kwa asilimia 95

Folz amesema leo jioni watakuwa na nafasi ya kukamilisha maandalizi hayo kuelekea mechi hiyo muhimu ya mkondo wa kwanza kuwania kufuzu hatua ya makundi ya CAFCL

Akizungumza katika mkutano na wanahabari mapema leo kuelekea mchezo huo, Folz alisema ana taarifa za kutosha kuhusu wapinzani wao Silver Strikers na hivyo ameiandaa timu yake kimkakati ili kuhakikisha wanapata matokeo mazuri

"Tumejiandaa vizuri kuelekea mchezo wetu wa kesho na leo jioni tutapata nafasi nyingine ya mwisho ya kukamilisha maandalizi."

"Tumeangalia historia ya wapinzani wetu na kufanya utafiti wa kiufundi kama tunavyofanya tukikutana na wapinzani wengine"

"Tunafahamu hautakuwa mchezo mwepesi lakini tunakwenda kupambana ili kuhakikisha tunapata matokeo ya ushindi," alisema Folz

Yanga itafanya mazoezi yake ya mwisho jioni katika uwanja wa Taifa wa Bingu ambao mchezo huo utapigwa hapo kesho saa 10 jioni

Akizungumza kwa niaba ya wachezaji wenzake, kiungo Duke Abuya amesema wako tayari na kwa kuzingatia maelekezo waliyopewa na Mwalimu, wana matumaini makubwa ya kuondoka na ushindi

"Kwa niaba ya Wachezaji wenzangu maandalizi ni mazuri na mchezo wa kesho kwetu ni muhimu na kutokana na maelekezo ya Kocha wetu tunaamini tutaondoka na matokeo mazuri," alisema

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
7h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
10h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
15h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’