Yanga kuifuata Silver Strikers Alhamisi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
14 Oct 2025
Yanga kuifuata Silver Strikers Alhamisi

Kikosi cha Yanga siku ya Alhamisi, Oktoba 16 kitaondoka jijini Dar es salaam kuelekea Malawi tayari kwa mchezo wa mkondo wa kwanza kuwania kufuzu hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya Silver Strikers

Jumamosi Oktoba 18, Yanga itakuwa ugenini dimba la Bingu kumenyana na wenyeji wao katika 90 za kwanza kuwania kutinga hatua ya makundi

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amesema kikosi kitaondoka nchini siku ya Alhamisi na kuwasili Malawi siku hiyohiyo

Yanga itakuwa na siku moja ya kukamilisha maandalizi yake nchini Malawi kuelekea mchezo huo ambao utapigwa saa 10 jioni kwa saa za Tanzania huko Malawi ikiwa ni saa 9 Alasiri

"Timu inaendelea na maandalizi Avic Town ambapo jana kikosi kiliingia rasmi kambini. Tunatarajia kuondoka nchini siku ya Alhamisi, tayari kwa mchezo ambao utapigwa siku ya Jumamosi," alisema Kamwe

Aidha amesema msafara wa mashabiki utaondoka nchini siku ya kesho Jumatano ambapo mpaka sasa mabasi 40 yamethibitishwa kubeba mashabiki kuelekea Malawi

Kamwe amewataka mashabiki kuendelea kuchangamkia fursa hiyo ya kusafiri Malawi kuiongezea hamasa timu yao ambapo lengo ni kuingia Malawi na mabasi yasiyopungua 50

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
4h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
7h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
12h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
16h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’