Mchezo wa mzunguuko wa 29 ligi kuu ya Vodacom kati ya Yanga dhidi ya Ruvu Shooting umemalizika kwa timu hizo kugawana pointi baada ya kutoka sare ya mabao 2-2.
Mchezo huo uliopigwa uwanja wa Uhuru uliishuhudia Yanga ikitangulia kupata bao la kuongoza kupitia kwa Matheo Antony kwenye dakika ya 19 kabla Hamis Mcha hajaisawazishia Ruvu Shooting kwa mkwaju wa penati kwenye dakika ya 30.
Hata hivyo mkwaju huo wa penati ulikuwa na utata mkubwa kwa kuwa beki Abdallah Shaibu aliyehusika katika adhabu hiyo hakuonekana kuunawa mpira.
Yanga iliongeza bao la pili kwenye dakika ya 39 kupitia kwa kiungo wake anayekuja juu Maka Edward kwa shuti kali baada ya kupasiana 'kampa-kampatena' na Pius Buswita.
Ruvu Shooting wakasawazisha kwenye dakika za mwanzo za kipindi cha pili kupitia kwa Issa Kanduru.
Matokeo hayo yanaifanya Yanga iendelee kubaki nafasi ya tatu baada ya kufikisha alama 52 na inahitaji ushindi kwenye mchezo dhidi ya Azam FC ili kuwaondoa wana rambaramba hao kwenye nafasi ya pili.

ADVERTISE HERE