Folz apewa dakika 180 kuivusha Yanga makundi CAFCL

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
13 Oct 2025
Folz apewa dakika 180 kuivusha Yanga makundi CAFCL

Baada ya tetesi za Yanga kumalizana na mkufunzi wa timu ya Taifa ya Madagascar Romuald Rakotondrabe 'Roro' na sasa ikielezwa kuna mazingira yameweka ugumu kwa Yanga kumpata Roro kwa wakati huu, Mkufunzi wa Yanga Romain Folz anaendelea na majukumu yake kama kawaida

Folz amekadhiwa jukumu la kuivusha Yanga hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa akikabiliwa na dakika 180 mbele ya Silver Strikers ya Malawi

Mchezo wa mkondo wa kwanza utapigwa Oktoba 18 na marudiano kupigwa Oktoba 25 jijini Dar es salaam

Ni takribani siku tano tu zimesalia kuelekea mchezo huo, ni wazi haitawezekana Yanga kufanya mabadiliko ya benchi la ufundi sasa

Unaweza kusema Folz amepewa nafasi nyingine ya kuwashawishi mashabiki ambao kimsingi ndio wanaopeleka presha kwa uongozi afutwe kazi

Dakika 180 za mchezo dhidi ya Silver Strikers zinaweza kubadili upepo na kocha huyo kuendele kusalia Jangwani

Lakini kama mambo yatakwenda tofauti hata katika mechi ya mkondo wa kwanza itakayopigwa Jumamosi huko Malawi, uongozi unaweza kulazimika kuchukua uamuzi mgumu na pengine kuteua kocha wa muda wakati wakiendelea kusubiri hatma ya Roro

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
8m ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
47m ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
4h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
5h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
15h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
15h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
18h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
23h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’