Kocha Mkuu wa Yanga Princess Edna Lema amesema kikosi chake kiko tayari kwa mchezo wa nusu fainali ya Ngao ya Jamii dhidi ya JKT Queens ambao utapigwa kesho Alhamisi katika uwanja wa KMC Complex
Akizungumza kwenye mkutano na wanahabari mapema leo, Lema alisema msimu huu ana kikosi imara zaidi na dhamira yao ni kwenda kushindani kila taji
Lema amesema wanawaheshimu JKT Queens kwa sababu ndio mabingwa wa ligi kuu ya Wanawake pia wakitwaa Ngao ya Jamii msimu uliopita lakini hawawaogopi
"Tutakuwa na mchezo mgumu JKT Queens ni timu nzuri na inafanya vizuri ni mabingwa watetezi wa ligi ya wanawake pia upande wa CECAFA, na sisi tumejiandaa vizuri kuhakikisha kwamba tunafanya kile kinachotakiwa na kupata matokeo mazuri"
“Kama timu hatuwezi kuwa na presha sababu nimetengeneza timu vizuri, tunakuja kwa kuwaheshimu JKT Queens na sio kuwaogopa”
“Kuna project mpya ambayo kwenye team tunayo tulimaliza msimu tukiwa na matokeo mazuri na timu ilizidi kuwa bora, na msimu uliopita JKT Queens walichukua ngao katika mechi ya fainali tukiwa pamoja na awamu hii tumejiandaa vizuri kupata matokeo kuhakikisha tunaanza msimu mpya kwa ubora zaidi,” alisema